TRA

TRA

Monday, September 4, 2017

Yusuf Manji afikishwa mahakamani ghafla

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Leo September 4 2017 haikuwa tarehe iliyotajwa ya mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu kufika mahakamani  lakini amefikishwa mahakama ya hakimu makazi Kisutu ili itolewe ruhusa ya Manji na wenzake watatu kuhojiwa na Polisi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Mahakàma ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu Manji na wenzake watatu wahojiwe na Polisi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema ameruhusu washtakiwa wahojiwe baada ya kuandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi (ZCO)…

"Hivyo nikisema mahakama izuie wasihojiwe itakuwa tunapingana nao, wakati kila siku tunapigiana kelele kuhusu upelelezi kukamilika. Hivyo sifikirii kesi hii kila siku iwe inatajwa tu," alisema.

Hakimu Shahidi alimkabidhi Manji na washtakiwa wenzake kwa Koplo Dotto ambapo amemtaka hadi kesho kwenye muda wa kazi wawe wamerudishwa mahakamani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger