Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito kwa serikali ya
Afghanistan kushughulikia kitisho kinachosababishwa na kundi la Taliban,
al-Qaeda na makundi mengine yenye mafungamano na kundi la itikadi kali
linaojiita Dola la Kiisilamu yanayotishia usalama na uthabiti wa nchi
hiyo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisistiza juu ya
kuendelea kuiunga mkono Afganistan katika suala la ulinzi na usalama
ikiwa ni pamoja na juhudi za nchi hiyo za kupambana na ugaidi. Kundi la
Taliban ambalo limekuwa likiendeleza uasi kwa zaidi ya miaka 15 dhidi ya
serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono na Marekani lilifanikiwa
kudhibiti maeneo kadhaa nchini humo katika kipindi cha mwaka 2016 wakati
vikosi vya Afghanistan vikijitahidi kupambana na wanamgambo hao tangu
pale majeshi ya Marekani na yale ya NATO yalipohitimisha operesheni yao
ya awali mwishoni mwa mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment