TRA

TRA

Tuesday, April 18, 2017

Wagombea wakuu Ufaransa wafanya mikutano Paris

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Wagombea wawili wa urais wanaopewa nafasi kubwa katika uchaguzi ujao nchini Ufaransa, Emmanuel Macron na Marine Le Pen jana walifanya mikutano mikubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Paris kupigia debe sera zao.

 Akizungumza mbele ya umati wa watu 20,000 Macron mwenye sera za mrengo wa kati alisema anataka Ufaransa yenye kujiamini na kutetea msimamo wake wa kupendelea Umoja wa Ulaya. 



Macron ambaye aliwahi kuwa waziri wa uchumi, alisema anataka uhusiano wenye usawa na Ujerumani, siku chache baada ya kusema nguvu kubwa ya Ujerumani kiuchumi haikuwa yenye tija kwa ukanda unaotumia sarafu ya euro. 

Kwa upande wake Marine Le Pen wa siasa kali za kizalendo aliyehutubia kundi la watu 6,000, alisema uamuzi wake kama rais utakuwa kurejesha udhibiti wa mipaka ya Ufaransa mikononi mwa wafaransa na kuongeza kuwa uhamiaji hauleti fursa kwa Ufaransa.

 Wagombea watakaoongoza katika duru ya kwanza Jumapili ijayo watapambana katika duru ya pili tarehe 7 Mei.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger