Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nasor kushoto
akisaini Mkataba wa Ujenzi wa SERTILITE CITY ni kwa niaba ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na kulia ni Mwenyekiti wa Makapuni ya Bakhresa,
Said Salim Bakhresa akisaini kwa niaba ya Makampuni hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nasor kushoto
na Mwenyekiti wa Makapuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa
wakikabidhiana hati za Mkataba wa Ujenzi wa SERTILITE CITY mara baada ya
kusaini katika hafla iliyofanyika Fumba nje kidogo ya mji wa Zanzibar
Picha ya pamoja ya hafla ya
utiaji Saini Mkataba wa ujenzi wa Miundombinu ya Mji wa kisasa maarufu
kama “SERTILITE CITY” utakaojengwa huko Fumba nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar
Baadhi ya Nyumba zinazoendelea kujengwa katika Mji wa
kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” huko Fumba nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar chini ya Makapuni ya Bakhresa .
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 24.04.2017
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imetiliana Saini Mkataba na Makapuni ya Bakhresa kwa ajili ya
ujenzi wa Miundombinu ya Mji wa kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY”
utakaojengwa huko Fumba nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Chini ya Mkataba huo Makampuni
ya Bakhresa yatajenga Mji wa kisasa utakaobadili haiba ya nchi ambapo
kukamilika kwake kutaiwezesha Zanzibar kuwa na Majengo makubwa yenye
Goghofa zaidi ya 30 na Hotel zenye hadhi zaidi ya Nyota tano.
Waliotia Saini Mkataba wa Ujenzi
wa “SERTILITE CITY” ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega
uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor kwa niaba ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Makapuni hayo Said Salim Bakhresa
kwa niaba ya Makampuni hayo.
Akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa ZIPA Nassor ameeleza kuwa jumla ya Hekta 3,000 zimetolewa
na Serikali ili kufanikisha mradi huo ambao tayari majengo kadhaa
yameanza kujengwa.
Amefahamisha kuwa katika Mji huo
kutakuwa na Nyumba za kibiashara za kuishi watu,zenye ukubwa tofauti
kulingana na mitaa ambapo mitaa mingine zitafikia ukubwa wa zaidi ya
Ghorofa 30.
“Kutakuwa na majengo tofauti
kulingana na Maeneo, kutakuwa na Private Villa na katika high street
kutakuwa na ghorofa zaidi ya 30” alifafanua Mkurugenzi Salum
Ameongeza kuwa kutakuwa na
Kiwanja cha kimatifa cha Mpira wa Miguu na Viwanja vidogo vidogo, Kituo
cha Kibiashara, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano na Bandari ndogo
itakayounganisha Dar es Salaam na Pemba.
Kwa kweli itakuwa ni Mji wa
kivutio wa aina yake kwa Wenyeji na Wageni mbalimbali ambao bila shaka
watakuwa na shauku ya kutembelea na kupata huduma mbalimbali” alisema
Mkurugenzi ZIPA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Makampuni ya Bakhresa Salim Ali Salim amesema tayari wametenga kiasi cha
Dola Million 500 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya “Sertilite City”
katika hatua za awali huku gharama ikitarajiwa kuongezeka kulingana na
mahitaji ya baadae.
Aidha ameeleza kuwa manufaa
yatakayopatikana ni pamoja na nafasi za ajira 3,000 za moja kwa moja kwa
Wananchi jambo ambalo pia litabadili hali zao za kimaisha.
Awali Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar, Dkt Khalid Salum Mohammed amewahakikishia Mashirikiano ya
kila aina Wawekezaji hao Wazalendo na kuwaomba waendelee kuiunga Mkono
Serikali katika azma yake ya kuwaletea maendeleo Wananchi.
Amesema Sheria Namba 11 ya Mwaka
2004 inatoa nafasi kwa Serikali kuwalinda wawekezaji hasa Wazawa na
hivyo kuwaomba Wawekezaji wengine kuitumia Fursa Hiyo ili kuendelea
kuwekeza zaidi Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega uchumi Zanzibar (ZIPA)
imeweka mazingira salama ya kiuwekezaji hasa katika maeneo huru
yaliyotengwa ili Wawekezaji Wazawa na Wageni waendelee kuwekeza katika
maeneo hayo kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Mradi huo wa Ujenzi wa Mji wa
kisasa maarufu kama “SERTILITE CITY” huko Fumba utakuwa ni miongoni mwa
miradi mikubwa iliyowekezwa Zanzibar na Bakhresa ambayo itaendelea
kuisaidia Serikali ya Zanzibar kukuza kipato cha wananchi wake na Pato
la Taifa kwa ujumla.
SHARE
No comments:
Post a Comment