Mariam Zayumba akiwa mitamboni katika kiwanda cha TBL Mwanza.
…………………….
-Ni Fundi wa kutegemewa kiwanda cha TBL Mwanza
Mariam Zayumba (20) mmoja wa wahitimu wa mafunzo wa ufundi stadi fani ya umeme katika chuo vya VETA kupitia mpango maalumu wa elimu ya vitendo ambaye alipata
mafunzo kampuni ya TBL Group na kuajiriwa na kampuni hiyo baada ya
kuhitimu amepata nafasi ya mafunzo zaidi ya vitendo nchini Ujerumani
chini ya ufadhili wa serikali ya nchi hiyo.
Elimu
ya ufundi stadi kupitia mpango maalumu wa kupata elimu zaidi ya vitendo
kuliko nadharia unaojulikana kitaalamu kama Dual Apprenticeship
programme unaendeshwa na serikali kupitia taasisi zake za mafunzo ya
ufundi kwa kushirikiana na Chama cha Wenye Ujuzi cha Hamburg, Ujerumani,
umelenga kuwapatia vijana mafunzo ya vitendo ambapo wanasoma wakiwa
wanapatiwa mafunzo ya vitendo kwenye viwanda na taasisi mbalimbali na
kampuni ya TBL Group ni mdau mkubwa katika utekelezaji wa mpango huu.
Akiongea
kuhusiana na nafasi ya kujiendeleza zaidi nchini Ujerumani Mariam
alisema kuwa anashukuru wafadhili walioweza kumpatia fursa hiyo pia
mwajiri wake kampuni ya TBL Group ambapo ndio imemlea kwa kumfadhili
wakati wa masomo nakumpatia mafunzo ya vitendo ya ufundi umeme na baada
ya kufuzu mafunzo ya VETA iliweza kumpatia ajira ya kudumu akiwa ni
fundi umeme wa kampuni hiyo katika kiwanda chake cha Mwanza,
“Nitachowaahidi
watanzania wenzangu kuwa nitatumia fursa hii kupata ujuzi ambao
nikirudi nitautumia kwa manufaa ya watanzania na nashukuru TBL Group kwa
kunipatia mafunzo ya awali ambayo yameniwezesha kufikia hatua hii na
natoa wito kwa vijana wenzangu kujikita zaidi kwenye fani ya ufundi kwa
kuwa inazo fursa nyingi za ajira zinazowawezesha kuendsha maisha yao na
kuhudumia familia zao kama ambavyo imetokea kwangu”Alisema Mariam kwa furaha.
Meneja
Mafunzo wa TBL Group,Gaspar Tesha,amesema kuwa kampuni inajivunia kuwa
mmoja wa wadau wa mpango huu wa kutoa elimu ya ufundi stadi kwa vitendo
bila kuwa na elimu ya awali kwa kuwa ina manufaa makubwa kwa taifa
ikiwemo kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini.
“
“Kampuni yetu ikiwa ni moja ya mwajiri mkubwa yenye wafanyakazi wapatao 2,000 itaendelea kuwekeza katika program hii ya kuwawezesha
vijana kupata ajira na kujiajiri kupitia fani ya ufundi .Tunajivunia
mmoja wa wanafunzi wetu ambaye pia tumemwajiri ameweza kuwa miongoni mwa
wanafunzi waliofanya vizuri wakati wa mafunzo hayo awamu ya kwanza na
kufanikiwa kupata nafasi ya kupata mafunzo ya juu ya vitendo nchini
Ujerumani”.Alisema Tesha.
Aliongeza
kuwa kampuni katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo ilichukua wanafunzi
watatu na kuwagharamia kiasi cha shilingi milioni 75 za kujikimu wakati
wa mafunzo ambapo baada ya kuhitimu wamepata ajira ya kuduma katika
viwanda vyake na wanaendelea kufanya vizuri katika fani ya umeme na
wataendelea zaidi kuwezesha wanafunzi wengine zaidi wanaochaguliwa
kujiunga na mpango huu wa Dual Apprenticeship.
Mpango
huu tangu uanzishwe nchini umeishachukua wanafunzi katika awamu mbili
ambapo awamu ya kwanza ilikuwa kati ya mwaka 2013 hadi 2016 na awamu
nyingine inaendelea na mafunzo katika fani za umeme,ufundi magari,na
huduma za hoteli ambapo katika awamu ya kwanza TBL Group ilichukua
wanafunzi watatu na katika awamu ya pili wanafunzi 4.
SHARE
No comments:
Post a Comment