Rais Dk John Pombe Magufuli
akipokea ripoti kutoka kwa Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa
Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya
madini yaliyomo kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa
na Serikali Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini katika hafla
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 24/5/2017, Katikati
ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU DAR ES SALAAM)
Rais Dk John Pombe Magufuli
akipokea ripoti kutoka kwa Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa
Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya
madini yaliyomo kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa
na Serikali Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini hafla hiyo
imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 24/5/2017, Katikati
ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
……………………………………..
Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Mruma hii leo Ikulu!.
1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.
2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.
3. Hadidu za rejea zilikuwa
,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya Dar es salaam na
migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya
madini yaliyopo kwenye makinikia,kuchunguza uwezo wa scanner zilizopo
bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,
4.Kamati ilitembelea bandari ya
Dar es salaam,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na
Buzwagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na
chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.
5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.
6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.
MATOKEO YA UCHUNGUZI
1.Kamati imebaini uwepo wa
dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277
yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.
3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.
4.Copper pekee ilikuwa ya thamani
ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripoti ya
serikali ambayo ilionesha kuwa na thamani ya Bilioni 13.
4.Upande wa silver kamati
ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya
Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.
5.Upande wa surpher kamati
ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati
ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha
6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,
7.Kamati ilibaini uwepo wa madini
mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya
bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5
Thamani ya madini yote katika
makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana
thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na
hayapo kwenye mrabaha!.
8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.
9.Kamati imebaini wakala wa
madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya
madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha
makontena.
10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.
MAPENDEKEZO YA KAMATI
1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi
2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini
3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.
4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia
5.TMAA ipime viwango vyote vya
makinikia na madini kwenye maabara bila kujali ripoti ya msafirishaji
hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.
6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.
7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.
8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.
Rais Dk John Pombe Magufuli
akielekezwa jambo wakati akipokea ripoti ya ukaguzi kutoka kwa Profesa
Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi
ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga
uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali Bandarini na sehemu
mbalimbali hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam, Katikati ni Makamu
wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Rais Dk John Pombe Magufuli
akizungumza wakati akipokea ripoti ya ukaguzi wa madini katika
makontena hayo Katikati Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na
kulia ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan.
Profesa Abdulkarim Hamis
Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza Madini katika Mchanga
ulioko kwenye makontena ambayo yamezuiliwa maeneo mbalimbali nchini
akizungumza wakati wakiwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es salaam
leo
Rais Dk John Pombe Magufuli na
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan wakifuatilia kwa makini
wakati Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum
ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo
kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali
Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini alipokuwa akiwasilisha ripoti
hiyo.
Rais Dk John Pombe Magufuli ,
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mh. Kassim
Majaliwa wakifuatilia kwa makini wakati Profesa Abdulkarim Hamis
Mruma Mwenyekiti wa Kamati hayupo pichani alipokuwa akiwasilisha ripoti
hiyo.
Rais Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali mara baada ya kupokea ripoti hiyo.
Waimbaji Frora Mbasha, Kalala
Junior na Shilole pamoja na wenzao wakitumbuiza wimbo maalum wakati wa
kuwasilishwa kwa ripoti hiyo.
Wasanii mbalimbali wakitumbuiza wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hiyo Ikulu leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwapongeza wanasanii hao mara baada ya
kuimba wimbo maalum wa kuhamasisha uzalendo kwa nchi Iukulu leo.
Rais Dk John Pombe Magufuli akimpongeza MwanaFA na wenzake.
Rais Dk John Pombe Magufuli
akimpongeza Frola Mbasha na wenzake mara baada ya kuimba wimbo maalum wa
kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo mara baada ya kupokea ripoti
hiyo.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa srikali , Dini, vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla hiyo.
Wasanii mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu leo.
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wasanii
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na vion
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalaam Jenerari Venance Mabeyo akisalimiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Sheikh Al- Hadi Salum Musa
Picha mbalimbali zikionyesha Rais
Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali mara baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa Kamontena ya
Mchanga yaliyozuiliwa Bandarini na maeneo mbalimbali nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment