TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

Uingereza yakubali kuondoka kwa awamu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Baada ya siku ya kwanza ya mazungumzo mjini Brussels, Ubelgiji, Uingereza imekubali mpango wa Muungano wa Ulaya wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo kwa hatua. 

Waziri wa Uingereza anayeongoza mpango huo David Davis, amekubali kusitisha mazungumzo kuhusu mikataba ya kibiashara kati ya pande hizo mbili hadi hatma ya raia wa pande hizo walioko mataifa ya EU na fidia ya mwisho ya utengano kuafikiwa.
 Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya BREXIT

Aidha amesema ni wazi kwamba pande zote mbili zinataka kupata kustakabali mzuri wa uhusiano wao.
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo Michel Barnier amesema kwa pande zote mbili Umoja wa Ulaya na Uingereza makubaliano ya haki yanawezekana na ni bora zaidi kuliko kutofanya kabisa.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger