Waziri wa Elimu
nchini Kenya, Dk Fred Matiang'i ameteuliwa kuwa Kaimu Waziri wa Usalama
wa Ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph
Nkaissery.
Uteuzi wa Dkt Matiang'i umetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama wa Taifa.
Rais Kenyatta amesema hakutakuwa na pengo lolote kiusalama nchini kutokana na kifo cha jenerali huyo mstaafu.
Rais amesema maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 Agosti, mwezi mmoja kuanzia sasa, yataendelea bila kuvurugika. Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kudumisha utulivu.
SHARE
No comments:
Post a Comment