Mahakama kuu nchini Kenya
imefutilia mbali zabuni ya jumla ya $24m (£18m) ya uchapishaji wa
karatasi za kura ya urais nchini humo.
Upinzani
ulikuwa umesema kampuni iliyopewa kandarasi hiyo ina uhusiano na Rais
Uhuru Kenyatta amabye pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika
tarehe 8 Agosti.
Mahakama imeamua kuwa zabuni hiyo itangazwe upya.
Muungano mkuu upinzani National Super Alliance (Nasa), ulikuwa umewasilisha kesi kortini ukisema kampuni hiyo ilipewa zabuni hiyo bila utaratibu ufaao kufuatwa.
Tume ya uchaguzi ilikuwa imesema ilifuata utaratibu ufaao.
Kampuni ya Al Ghurair na Bw Kenyatta wote walikana kuwa na uhusiano wowote.
Mahakama iliamua kwamba kampuni hiyo inaweza kuchapisha karatasi za uchaguzi wa wabunge na maseneta, madiwani na magavana, ambao pia utafanyika tarehe 8 Agosti.
Mgombea urais wa Nasa Raila Odinga anashindana vikali na Rais Kenyatta, katika kinyang'anyiro ambacho ni kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2013. Odinga anawania urais kwa mara ya nne.
SHARE
No comments:
Post a Comment