Lowassa Aripoti Polisi…..Atakiwa Kurudi Tena Alhamisi Ijayo
0
Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuwasili katika ofisi
ya mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, kama alivyotakiwa kufanya
Juni 29, ameruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi tena Alhamisi ijayo.
Mwanasheria wa Lowassa, Peter Kibatala amezungumza na waandishi wa
habari na kusema kuwa Lowassa ametakiwa kurudi Alhamisi bila sababu za
kuahirishwa kwa mahojiano hayo kuwekwa wazi.
“Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi,” alisema
Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.
Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni
28 na Juni 29 na Wakili Kibatala alizungumza na wanahabari mara baada ya
mahojiano hayo.
Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23, mwaka huu katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
SHARE
No comments:
Post a Comment