Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte
Meya wa
jiji la Ozamiz nchini Ufilipino, Reynaldo Parojinog ambaye anatuhumiwa
na Rais wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte kuwa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya ameuawa katika msako wa Jeshi la Polisi.
Reynaldo
Parojinog ameuawa kwa kupigwa risasi pamoja na mkewe na watu wengine 10 nyumba yake ilipovamiwa na askari.
Polisi wanasema walikuwa
wakisaka katika nyumba hiyo, kukabidhi waranti ya kumkamata Meya huyo
ndipo utumiaji nguvu ukazuka.
Watu
karibia elfu 9 wameshauawa katika misako ya polisi, au wameuliwa na
magenge ya wanamgambo, tangu Rais Duterte kuingia madarakani mwaka jana,
kufuatia kampeni ya uchaguzi, ambapo aliahidi kuua maelfu ya watu ili
kufyeka biashara ya mihadarati nchini Ufilipino.
Katika
msako huo Polisi walipata bunduki, pesa na madawa ya kulevya kwa mujibu
wa mkuu wa polisi wa Ozamiz, Kamanda Jaysen De Guzman.
Bwana
Porojinog ni Meya wa tatu kuuawa katika harakati kali za Serikali
kukabiliana na madawa ya kulevya, ambapo Rais Duterte amewataja maafisa,
polisi na majaji kuhusika kwenye biashara hiyo.
Hatua
hiyo imempa umaarufu Rais Duterte duniani ingawaje imekoselewa na
makundi ya kupigania haki za binadamu ulimwenguni kwa kukemea kitendo
hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment