Msichana
mkazi wa Texas, Marekani ambaye alikimbilia kanisani na kudai kuwa
amebakwa na kundi la wanaume watatu wenye asili ya Afrika, huenda
akahukumiwa kifungo jela baada ya kukiri kwamba alidanganya.
Breana
Harmon, mwenye umri wa miaka 19, mapema mwezi March alikimbilia Kanisani
mjini Denison, Texas, akiwa na nusu uchi na mwili wake ukiwa damu na
kudai kubakwa na wanaume wawili wakati mwingine akimshikilia chini,
unaripoti mtandao wa KXII.
Hata
hivyo, vipimo vya Hospitali havikuonesha ushahidi wowote kuwa msichana
huyo alidhalilishwa na wanaume hao wenye asili ya Afrika ambapo wiki
mbili baada ya tukio hilo alikiri kwa Polisi kuwa alidanganya juu ya
tukio hilo na kuumia kwake kulitokana na yeye mwenyewe.
Kwa
mujibu wa Mwanasheria Joe Brown, msichana huyo alifunguliwa kesi ya
jinai mapema wiki hii kutokana na kudanganya ambapo thamani ya kosa ni
kifungo cha hadi miaka 10 jela na faini ya Dollar 10,000.
“Tulivyoangalia
katika kilichotokea kwenye kesi hii, na kuzingatia madhara
iliyosababisha, na pengine itakayosababisha, tunaamini alichokifanya
kinastahili adhabu zaidi. Alichokifanya ni kikubwa, na tunaamini ilikuwa
ni kosa la jinai,” – Joe Brown.
SHARE
No comments:
Post a Comment