STAA wa filamu za Kibongo toka kitambo, Blandinda Chagula ‘Johari’ ametema
cheche kuwa hata kama ametumika muda mrefu kwenye tasnia hiyo lakini
bado anaheshimika kwa mashabiki wake na siyo ‘Used’ kama wanavyodai
mastaa wanaochipukia.
Akizungumza na ilikuwa
ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, alisema anaamini yeye kama staa
aliyekuwa akisumbua huko nyuma anapotumia akili au kuweka jambo lolote
kwenye filamu hata kama hataicheza yeye bado itakuwa na ladha nzuri ya
kipekee.
“
Yaani utasikia hawa mastaa wapya wanapenda kutuita sisi ni ‘Used’
lakini ukweli ni kwamba japokuwa wanatuita hivyo ladha ya mastaa wa
zamani ni tofauti na wa sasa, kuna vitu ukiviangalia hatuwezi kulingana
kabisa,” alisema Johari.
SHARE
No comments:
Post a Comment