Mtandao mpya unaoundwa na Radio na
vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya
habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA
DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya
kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA.
Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao
pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo.
Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina
la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi
mwezi machi mwaka huu.
Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga
kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine
vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii
kwa ajili ya maendeleo. Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.[/caption]
Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania,
ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo Bw. Christophe Legay kwa
niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua
iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya.
Alieleza kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na shirika
hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma
sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea
maendeleo ya upashanaji wa habari nchini.
Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa
kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini. Mwenyekiti
mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe mara
baada ya uchaguzi. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya TADIO,
Maimuna Msangi na Katibu Mtendaji wa TADIO, Marco Mipawa.[/caption]
Aliwaasa kushughulika na masuala ya kibinadamu na si watu binafsi.
Wakati huo huo Mtandao huo unaoundwa na jumla ya Radio 32 kutoka katika
mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar, umefanya uchaguzi mkuu na
kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zake kwa miaka mitatu ijayo.
Uchaguzi huo ulitanguliwa na tukio la kujiuzuru kwa viongozi wa mpito
waliochaguliwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi
kuvunjika kwa muungano wa awali wa radio jamii wa COMNETA. Katibu
Mtendaji mpya wa TADIO, Marco Mipawa (kulia) akizungumza jambo mara
baada ya uchaguzi kufanyika. Kutoka kushoto ni Balozi Mstaafu Mh.
Christopher Liundi, Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO,
Ofisi za Tanzania, Christophe Legay, Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper
Kwigize na Mjumbe wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi.[/caption]
Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni mlezi wa
ushirika huo, Balozi mstaafu Mheshimiwa Christopher Liundi, alimtangaza
Bw. Prosper Kwigize aliyekuwa mgombea pekee kuwa Mwenyekiti mpya
baada ya kupata kura za ndiyo 26 kati ya kura 30 zilizopigwa na
wajumbe waliohudhuria.
Balozi Liundi, pia alimtangaza Bw. Marco Mipawa kuwa Katibu Mtendaji
baada ya kupata kura 28 za ndiyo, Aidha Mipawa pia alikuwa mgombea
pekee katika uchaguzi huo.
Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Mweka Hezina, Shaaban Ali
Makame aliepata kura 24 za ndiyo. Pia mkutano huo uliwachagua wajumbe
sita wa Bodi ya shirika hilo la TADIO ambao ni Maimuna Msangi kutoka
Pangani FM, Gladys Mapeka kutoka Radio Kilosa, Ali Mbarouk Omar kutoka
kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari wa Pemba (PPC), Ali Khamis kutoka
Adhana FM Zanzibar, John Baptist kutoka Dodoma FM na Anthony Masai
kutoka Triple A FM. Balozi
mstaafu Mh. Christopher Liundi (kulia) akimpongeza akimpongeza
Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize.[/caption]
Akizungumza baada ya kutangaza matokea hayo, Balozi Liundi aliitaka
safu ya uongozi mpya kuongoza kwa kufuata katiba na malengo ya
shirika hilo kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya wananchi kwa
kupitia kazi zinazofanywa na radio za kijamii.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa TADIO Bw. Prosper Kwigize
amewashukuru wajumbe kwa kuchagua safu mpya ya uongozi na kuahidi
kujenga ushirikiano mpya ambao utawezesha kufikiwa kwa malengo ya
kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya
kijamii.
Bw. Kwigize ametoa wito kwa wadau wengine hususani Radio za kitaifa,
magazeti, waandishi wa habari za mitandaoni (bloggers) Muungano wa
wamiliki wa vyombo vya habari MOAT, TAMWA, MISA, Baraza la Habari
Tanzania, Runinga na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani kushirikiana
na shirika la TADIO ili kutoa huduma stahiki kwa jamii. Balozi
mstaafu Mh. Christopher Liundi akimpa pongezi Katibu wa TADIO Bw. Marco
Mipawa (shati la kitenge) mara baada ya matokeo kutangazwa.[/caption]
Amehimiza pia serikali na taasisi zake kutoa ushirikiano kwa TADIO ili
misimamo, dira na malengo yanayoibuliwa na serikali yawafikie wananchi
kwa haraka kupitia muungano huo wa Radio za mikoani.
Amesisitiza kuwa, mtandao huo wa TADIO una ofisi na studio ya kisasa
ndani ya Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT makao makuu Kinondoni Dar es
Salaam ambako kazi ya ofisi na studio hiyo ni kuratibu shughuli za
mtandao pamoja na kuandaa vipindi ambavyo vitakuwa vikisambazwa kwa
radio wanachama.
Aliitaka safu ya uongozi mpya kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga
umoja na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili
kuyafikia malengo ya ushirika huo.
Mtandao wa TADIO unafadhiliwa na UNESCO chini ya mradi wa SIDA/SDC. Msimamizi wa uchaguzi huo mwanasheria Harold Sungusia (mwenye tai) akimpongeza Mwenyekiti mteule wa TADIO, Prosper Kwigize. Picha
ya pamoja ya viongozi wa TADIO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi
na Msimamizi wa uchaguzi huo Mwanasheria Harold Sungusia.
SHARE
No comments:
Post a Comment