Msanii
wa kuigiza Ayoub ambaye katika tamthilia ya 'Jambo na vijambo' anaigiza
kama Yesu amefunguka na kusema kuigiza kama Yesu katika tamthilia hiyo
inamletea shida kwa baadhi ya watu ambao siyo waelewa.Ayoub alisema hayo
alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNewz na kudai kuwa kuna wakati
hata majirani waligombana na mkewe na hawakutaka kusemeshana naye kwa
kuwa mumewe anamuuigiza 'Yesu'
"Hata mke
wangu kishagombana na watu kwa sababu tu ya mimi kuigiza kama Yesu,
wanamwambia mumewe anamgeza mtume wetu Yesu wetu kwa hiyo usinisemeshe,
mke wangu akaja kunipa mimi hizo habari nikabaki kucheka tu, lakini
katika ule u serious zaidi sijaona kama kumetokea tatizo kubwa mimi ni
muislam lakini yapo makanisa yananiita nikawasaidie kutengeneza kazi ya
sanaa baada ya kuniona kwenye kile kipindi, kwa hiyo wenyewe wakristo
ambao wamezama kwenye imani kuniona naigiza kama Yesu hawafikirii vibaya
sababu hata nachoigiza mle ndani kinaendana na yale aliyokuwa anatenda
Yesu, hivyo huwezi kuona amefanya jambo lolote baya yule muhusika wa
Yesu ambaye ni mimi" alisema Ayoub
Mbali na
hilo Ayoub anasema watu ambao wanakuwa na mtazamo hasi juu ya uhusika
wake kama Yesu ni wachache sana ukifananisha na wale ambao wanafurahia
kwani mambo mengi ambayo anafanya muhusika ni mambo ya msingi.
"Hata
ukiangalia kwenye ukurasa wa facebook wa EATV tukiweka post akitokea mtu
ambaye atazungumza vibaya juu ya 'character' Yesu wapo watu wengine
wanakuja kumsema sana na kumuelewesha vizuri juu ya uhusika wa Yesu, kwa
hiyo utaona watu wanaozungumza uzuri wanashinda kutokana na mazuri
ambayo muhusika amefanya" alisema Ayoub
Kipindi cha Jambo na Vijambo kinaruka kila Jumapili kuanzia saa 12:30 jioni katika ting'a namba moja kwa vijana EATV
SHARE
No comments:
Post a Comment