Donald
Trump na Vladimir Putin wamekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza
kabisa, na wakasalimiana kwa mikono huku mkutano wa G20 mjini Hamburg
ukuanza.
Viongozi
hao wa Marekani na Urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya
nchi hizo mbili ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia
uchaguzi mkuu wa Marekani.
Masuala
ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo
katika mkutano huo mkuu wa siku mbili.Kumeshuhudiwa maandamano katika
barabara nje ya eneo ambapo mkutano huo unafanyika.Mke wa rais wa
Marekani Melania Trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa
akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano.
Alikuwa
amepangiwa kufanya matembezi mafupi pamoja na wake wengine wa marais
wanaohudhuria mkutano huo.Lakini msemaji wake Stephanie Grisham amesema:
"Polisi wa Hamburg walikataa kuturuhusu tuondoke."
SHARE
No comments:
Post a Comment