Mwanamke
mmoja mkazi wa Bomarodi manispaa ya Morogoro Neema Monyo amekamatwa na
maafisa wa mamlaka wa usimamizi wa bima kanda ya kati (TIRA) kwa
kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa madai
ya tuhuma za kukutwa akiuza bima feki kinyume na taratibu kunakopelekea
kuikosesha serikali mapato.
Bi.Neema
amejikuta akiwa katika wakati mgumu mara baada ya mama mmoja
aliyeuziwa bima ambayo ilionekana kuwa ni feki kukamatwa katika
operesheni ya kukagua bima feki inayoendelea mkoani hapa kisha kumtaja
aliyemuuzia na kukamatwa na kuwekwa nguvuni.
Naye
mama aliyedai kuuziwa bima hiyo feki Flora Musiba amesema yeye wakati
ananunua hakujua kuwa nifeki na baada ya gari yake kukamatwa akawasaidia
maafisa hao kuwaonyesha aliyemuuzia.
Kwa
upande wake meneja wamamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) kanda
ya kati Stela Rutaguza amesema wamemkamata muuzaji huyo kisha
wanamfikisha katika kituo cha polisi kumfungulia mashita kwa uuzaji wa
bima feki.
No comments:
Post a Comment