Jenerali Joseph Ole Nkaissery
Na BBC
Waziri huyo amefariki dunia saa
chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen
kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
“Ni kwa huzuni kubwa na
mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa
Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema.
“Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.”
Jenerali Nkaissery amefariki
siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa
jimbo la Laikipia kufariki dunia.
SHARE
No comments:
Post a Comment