Star wa Brazil Ronaldinho amenusurika kifo nchini India baada ya nguzo ya taa ya barabarani ya kuongozea magari kudondoka njiani na kuziba njia futi chache kutoka lilipokuwa gari ambalo limembeba Star huyo aliyewahi kutamba na timu ya Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Brazil.
Ronaldinho alikwenda India kwa ajili ya kuzindua mashindano ya mpira wa miguu (Sait Nagjee football tournament) na alikuwa njiani kutembelea moja ya shule kabla ya kukutwa na janga hilo.
Kundi kubwa la mashabiki waliokuwa wakilifuata gari hilo lilinyamaza wakati nguzo hiyo yenye kutu ilipoanguka na kuikatiza barabara. Shukrani za pekee ziwaendee polisi walioibeba nguzo hiyo kwa mikono kuiondoa barabarani kisha msafara wa Ronaldinho ukaendelea na safari.
Angalia video hapa jinsi Ronaldinho alivyonusurika
SHARE
No comments:
Post a Comment