TRA

TRA

Sunday, January 31, 2016

JAJI MKUU MHE MOHAMED CHANDE .OTHMAN AFUNGUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI MWAKA 2016

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.


Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Wanachi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila ( wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya  Watendaji na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Mahakama, Wakuu wa Idara  na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa tatu kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza leo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Mahakama ya Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watumishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger