Makazi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto
****
Washambuliaji ambao bado idadi yao kujulikana wanadaiwa kushambulia makazi ya vijijini ya Naibu Rais wa Kenya, William Ruto mjini Sugoi.
Namna walivyoingia makazi hayo ambayo yana ulinzi mkali ni kama filamu
iliyopangwa ikapangika vizuri, kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini
Kenya washambuliaji hao walitafuta namna ya kuingia katika lango kuu la
jumba hilo wakashindwa ikabidi watumie akili ya kuhadaa wana usalama
waliopo eneo hilo.
Ili wasishtukiwe kirahisi walimtuma mmoja wao kwenda getini akiwa
amebeba bidhaa kadhaa za nguo akiijifanya ni muuzaji wa nguo hizo, kwa
kuwa alikuwa ameshika nguo hizo wanausalama walimpuuza wakijua ni
muuzaji wa nguo.
Mtu huyo alisimama getini na kumwita afisa usalama
aliyekuwa getini na silaha na kumwambia anauza nguo.
Mara baada ya mwanausalama huyo kufika jamaa huyo aliyejifanya muuza
nguo alimkamata na kumnyang'anya silaha yake akamfyatulia risasi mbili
moja begani na nyingine kichwani.
Papo hapo washambuliaji waliojihami
kwa silaha walifika langoni hapo na kuingia ndani huku wakifyatua risasi
ovyo ndani ya nyumba hiyo.
Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni ya kupambana na
washambuliaji hao huku ikiwa bado kujulikana sababu ya mashambulisi hayo
katika nyumba ya kiongozi mkubwa katika nchi.
Imebainika kuwa watu hao walikuwa wakimsubiri Naibu wa Rais Willium Ruto
atkitoka na gari kwenda katika kampeni ili wamshambulie, lakini baada
ya kusubiri kwa muda mrefu bila kiongozi huyo kutoka wakaamua kuingia
kwa staili hiyo wakiwa na lengo la kumsaka Willium Ruto.
Kwa bahati nzuri kiongozi huyo aliamua kuondoka kwa helkopta kutokea
katika makazi yake na kuelekea katika eneo la mkutano wa kampeni, hii
ikawa bahati kubwa kwa kiongozi huyo wa Kenya kukumbwa na masaibu ambayo
yumkini yangeweza hata kuchukua uhai wake.
Vikosi vya usalama viliwasili dakika 15 baada ya mashambulizi hayo
kuanza na kuzingira nyumba hiyo ambapo milio ya risasi iliendelea
kusikika kwa zaidi ya saa mbili.
Hadi habari hii inaadikwa na kuingizwa
mtandaoni habari zinasema kuwa milio ya risasi kati ya maafisa usalama
na washambuliaji hao ilikuwa inaendelea kusikika.
Tukio hilo linatokea wakati Naibu Rais Wilium Ruto akiwa katika kampeni
zake za lala salama. Tukio hili linazidisha hofu kuhusiana na hali ya
usalama wakati huu wa uchaguzi ukikaribia.
SHARE
No comments:
Post a Comment