Rais wa Urusi
Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini
Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo
- Marekani yawafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi
- Bunge la wawakilishi Marekani launga mkono vikwazo dhidi ya Urusi
Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.
Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.
Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.
Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi. Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi.
SHARE
No comments:
Post a Comment