Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Simba, Evans Aveva, leo
Jumatatu wanatarajia kupanda tena mahakamani kwa ajili ya kusikiliza
kesi zao zinazoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Marais hao
wanatuhumuiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha ambapo
wote wapo mahabusu kutokana na kunyimwa dhamana.
Washtakiwa wengine
ambao wapo sambamba na kina Malinzi ni pamoja na Katibu wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Fedha TFF,
Nsiande Isawafo Mwanga pamoja na Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange
‘Kaburu’.
Kesi ya Malinzi na
Mwesigwa inasikilizwa chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wibroad Mashauri huku
kesi ya kina Aveva na Kaburu ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria
Nongwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment