Hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na klabu
ya Mbeya City Raphael Daud ameingia mkataba wa miaka miwili na Mabingwa
wa Kihistoria Yanga ambaye anatajwa kuwa Mbadala wa Haruna Niyonzima
ambaye amehamia Simba.
Msimu uliopita akiwa
Mbeya City alifunga jumla ya magoli nane na sasa amekamilisha usajili
wake rasmi na tayari amejiunga na kambi ya Yanga ambayo ipo mkoani
Morogoro na kesho ataanza mazoezi pamoja na mshambulizi Donaldo Ngoma
aliyejiunga leo.
Yanga imepiga kambi ya
Siku kumi na inatarajia kurejea Agosti 4 na itacheza mechi yake ya
kwanza dhidi ya matajiri wa Singida timu ya Singida United iliyochini ya
kocha wa Zamani wa Yanga,Hans Van Der Pluijm na mchezo utachezwa
Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Agosti 6.
SHARE
No comments:
Post a Comment