TRA

TRA

Monday, July 31, 2017

Sakata la kukwepa kodi, Ronaldo kufika mahakamani leo

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Cristiano Ronaldo anatarajiwa kufika mahakamani nchini Uhisipania leo baada ya kulaumiwa kwa kukwepa kulipa kodi.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa Ronaldo ambaye ni mcheza soka anayeripotiwa kulipwa fedha nyingi zaidi duniani, alikwepa kulipa kodi ya dola milioni 17.3 tangu mwaka 2010.

Nyota huyo wa Real Madrid amekana madai hayo.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 ni mwanasoka wa hivi punde kuchunguzwa na mamlaka za kukusanya ushuru nchini Uhispania.


   Cristiano Ronaldo
Muargentina Lionel Messi ambaye anachezea klabu ya Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa kama hayo mwaka uliopita.

Mapema mwaka huu mahakama iliamua kuwa atalipa Euro 232,000 badala ya kufungwa.

Hata hivyo Messi alilaumiwa kwa kutolipa Euro milioni 4.1 tu chini ya zile Ronald anadaiwa na atatoa ushahidi mahakamani mjini Madrid leo Jumatatu.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger