TRA

TRA

Monday, July 31, 2017

Samatta ameanza msimu wa 2017/18 Ubelgiji kwa kishindo

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana Samatta Jumamosi ya Julai 29 aliingia uwanjani kuichezea timu yake ya KRC Genk katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2017/18 dhidi ya Waasland Beveren.

KRC Genk leo imecheza game yake ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Waasland Beveren na kulazimishwa sare ya kufungana magoli 3-3, magoli ya Genk yakifungwa na Jose Naranjo dakika ya 70, Mbwana Samatta dakika ya 80 na dakika ya 82 Shrivjers akafunga goli la mwisho.

Magoli ya Waasland yamefungwa na Olivier Myny dakika ya 45, Zinho Gano dakika ya 47 na 90, sare hiyo sasa inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa timu hizo toka zilipokutana mara ya mwisho February 7 2017 na kutoma sare tasa, Genk na Waasland zote baada ya sare ya leo zinashika nafasi ya nne zikilingana kila kitu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger