WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani
Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo
na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.
Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa
takriban mwaka mmoja zmesababisha Madiwani hao kushindwa kufanya vikao
jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika
Halmashauri hiyo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumamosi, Julai 29, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani
Mbeya.
Amesema ikifika Jumatatu (Julai,
31, 2017) Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa
Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee
kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.
“Baraza la Madiwani limegawanyika
mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya
shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. Mkiendeleza
migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo wa tutalivunja baraza.”
Amesema baadhi ya Madiwani hao
wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiibia
Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki na halivumiliki.
“Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla sijaondoka.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya
kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma
wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu
za Serikali(CAG).
Pia aliwahasa watumishi wa umma
kuhakikisha wanatimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu kwa kufanya
kazi kwa bidi na kuacha ubabaishaji na kufanya kazi kwa mazoea na badala
yake wawahudumie wananchi ipasavyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 29, 2017
SHARE
No comments:
Post a Comment