Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, (kulia), akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya
Udhibiti Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA) kwenye jengo la Wizara ya
Fedha na
Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar
es Salaam, wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam. Wanaomsikiliza wakwanza kulia, ni Meneja wa Usimamizi na Utawala
wa Mifumo ya TEHAMA wa PPRA, Bw.Bernard Ntelya na Afisa
Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bw. Mcharo Mrutu.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, imeipongeza Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi katika sekta ya Umma
(PPRA), kwa kuisaidia serikali kuziba yanya ya upotevu wa fedha na
uonevu uliokuwa ukifanywa katika manunuzi kwenye sekta ya umma, lakini
akaishauri itoe elimu zaidi kwani watu wengi wakiwemo maafisa wa
serikali bado hawajaelimika vya kutosha kuhusu wajibu wa kuitumia na
kufuata taratibu za PPRA.
Waziri aliyasema hayo wakati
alipotembelea banda la Mamlaka hiyo ambayo inashiriki maonesho ya 41 ya
biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Dkt. Mpango alisema "Mnafanya kazi nzuri
sana kwa hivi sasa, lakini mnatakiwa kuongeza juhudi katika kuelimisha
kuhusu umuhimu wa kufuata taratibu za manunuzi katika sekta ya umma."
Alisema Dkt. Mpango.
PPRA imeanzishwa kwa sheria ya manunuzi ya Umma CAP 410 kama ilivyobadilishwa
na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya namba 7 ya mwaka 2011 ambayo inatoa Mamlaka ya
kusimamia manunuzi ya umma kwa taasisi zote za Umma (Serikali), upande wa Tanzania
Bara.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akitazama vipeperushi vyenye taarifa za Mamlaka hiyo.
Waziri Dkt. Mpango akiwa na Mkuu wa
Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja,
(wapili kulia), wakatinakianza kutembeela banda hilo.
Meneja wa Usimamizi na Utawala wa Mifumo
ya TEHAMA wa PPRA, Bw.Bernard Ntely(kulia), akimsikiliza Mwananchi
huyu aliyetembelea banda la Mamlaka hiyo ili kupata ufafanuzi wa
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment